Posts

Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma), Chanzo, Dalili na Tiba

Image
Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles. Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu. Kutokana na  kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.   Makundi ya Pumu Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili; Pumu ya ghafla (Acute asthma):  Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali...

Asthma(Pumu)

Image
Utangulizi   Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles.   Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya  kupitishia hewa  (bronchioles tubes)  hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito  (mucus)  na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa  nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.   Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease  . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.  Makundi ya Pumu Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili;   Pumu ya ghafla  (Acute asthma) : Wagonjwa...

FOMU YA RUFAA YA MATOKEO YA MTIHANI

Image
FOMU YA RUFAA YA MATOKEO YA MTIHANI

Tazama fly over ya Tazara ilivyokimbiza ujenzi na huu ndio muonekano wake

Image
Leo August 2,2018 tunayo story kuhusu muonekano wa sasa wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la TAZARA Jijini Dar es salaam. Barabara hii ya juu itakuwa ya kwanza hapa nchini na ujenzi wake umegharimu takribani Shilingi Bilioni 100 ambapo inatarajiwa kuzinduliwa September 2018 na Rais John Pombe Magufuli. Barabara hii itakuwa na njia 4 na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam. Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kunatarajia kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam. Mbali ya barabara hii pia Dar es Salaam itakuwa na barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo.

Hakuna mwanaume rijali anayeweza kitaka wa na mwanamke mmoja

Image
Kwa wale nitakaowakwaza naomba mniwie radhi lakini kweli hata mimi hainipendezi kuyasema haya ila ni vema tu niwaeleze dada zangu kwasababu ukweli unaoumiza ni bora, kuliko uongo unaofurahisha. Hakuna mwanaume riijali anayeweza kuwa na mwanamke mmoja, eidha awe ameoa au hata kama hajaoa. Hakuna mwanaume wa aina hiyo Karne hii, usijidanganye kukimbilia kwenye ndoa ukiamini kwamba baada ya kuolewa utajimilikisha huyo mwanaume aliyekuoa, never. "Mchele mmoja mapishi mbalimbali", utakuta wewe mwanamke kila siku ukikutana na jamaa yako faragha lazima yeye ndio aombe kamchezo, wakati kuna sehemu akienda mwanamke mwenzako ndio anaandaa mazingira ya kuomba kamchezo kutoka kwa jamaa, now u see the difference. Mara zote mkitoka lazima wewe ndio uwe ume suggest mtoke tena yeye ndio ana pay bills, wakati kuna mwanamke mwenzio some where ingawa sio mara zote, ila mara chache chache yeye ndio anamuomba jamaa watoke na ndio ana pay bills, umeona. Humshauri jamaa hata kununua an asset, ...

Mwalimu mkuu auliwa kwa kuchomwa na kisu mbele ya Wanafunzi

Image
MWALIMU mkuu wa shule moja ya sekondari  Jumapili iliyopita alivamiwa na kundi la watu sita akiwa darasani akachomwa na kukatwakatwa kwa visu hadi kifo chake. Hili lilifanyika mbele ya wanafunzi wake 20 aliokuwa nao darasani katika shule inayojulikana kama Havanur Public School ya huko Bengaluru, Jimbo la Karnataka, India, polisi wamesema. Mmoja wa wauaji hao alikamatwa baadaye  na polisi katika eneo la Mahalaxmi Layout baada ya kudokezwa na raia wema.  Mtu huyo alijeruhiwa mguuni baada ya polisi kumrushia risasi kufuatia jaribio lake la kuwashambulia.  Baadaye mtu huyo alipelekwa hospitali. Mwalimu huyo aliyekuwa anaitwa Ranganath (60),  akiwa mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyoko eneo la Agrahara Dasarahalli, alikuwa anaendesha masomo kwa wanafunzi wa darasa la kumi alipovamia na kundi hilo na kuuawa. Watu hao baadaye walitoroka katika gari dogo walilokuwa wemekwenda nalo shuleni hapo, walisema polisi. Polisi wanatuhumu mgogoro wa ardhi unaoihusisha shule hiyo...

KUISHI UKWELI  WA MWALIMU

Image
LICHA ya Mwasisi wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, kuwaacha Watanzania kwa takribani miongo miwili, maono yake mengi yanaendelea kuishi na kudumishwa na awamu ya tano. Hivyo hata kama Mwalimu angefufuka leo, akifurahia muendelezo wa maono yake na mafanikio makubwa yaliyofikiwa. Katika kumkumbuka Mwalimu. Nipashe, inazungumza na Mchumi na Mchambuzi wa masuala ya kijamii na maendeleo , Dk. Hoseana Lunogelo, kuangalia jinsi kazi za Mwalimu zinavyoakisiwa katika serikali  ya awamu  ya tano. Anaanza kwa kutaja baadhi ya mambo akisema mojawapo ya  kitu ambacho Nyerere alikiota ni suala la kila Mtanzania kupata elimu ili kufuta ujinga , kujiepusha na maradhi na kujiondoa kwenye umaskini. Anasema maono ya Mwalimu ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu yameendelea kuishi tena kwa kurejea sera ya elimu ya bure. Nyerere akiiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1961 hadi 1985, alisimamia sera ya kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania ili kila mmoja  asome.  Kwa ku...