Tazama fly over ya Tazara ilivyokimbiza ujenzi na huu ndio muonekano wake

Leo August 2,2018 tunayo story kuhusu muonekano wa sasa wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la TAZARA Jijini Dar es salaam.

Barabara hii ya juu itakuwa ya kwanza hapa nchini na ujenzi wake umegharimu takribani Shilingi Bilioni 100 ambapo inatarajiwa kuzinduliwa September 2018 na Rais John Pombe Magufuli.

Barabara hii itakuwa na njia 4 na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam.

Kukamilika kwa ujenzi wa barabara hii kunatarajia kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam.

Mbali ya barabara hii pia Dar es Salaam itakuwa na barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.