Mwalimu mkuu auliwa kwa kuchomwa na kisu mbele ya Wanafunzi

MWALIMU mkuu wa shule moja ya sekondari  Jumapili iliyopita alivamiwa na kundi la watu sita akiwa darasani akachomwa na kukatwakatwa kwa visu hadi kifo chake. Hili lilifanyika mbele ya wanafunzi wake 20 aliokuwa nao darasani katika shule inayojulikana kama Havanur Public School ya huko Bengaluru, Jimbo la Karnataka, India, polisi wamesema.

Mmoja wa wauaji hao alikamatwa baadaye  na polisi katika eneo la Mahalaxmi Layout baada ya kudokezwa na raia wema.  Mtu huyo alijeruhiwa mguuni baada ya polisi kumrushia risasi kufuatia jaribio lake la kuwashambulia.  Baadaye mtu huyo alipelekwa hospitali.

Mwalimu huyo aliyekuwa anaitwa Ranganath (60),  akiwa mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyoko eneo la Agrahara Dasarahalli, alikuwa anaendesha masomo kwa wanafunzi wa darasa la kumi alipovamia na kundi hilo na kuuawa. Watu hao baadaye walitoroka katika gari dogo walilokuwa wemekwenda nalo shuleni hapo, walisema polisi. Polisi wanatuhumu mgogoro wa ardhi unaoihusisha shule hiyo kuwa ndiyo chanzo cha tukio hilo.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU