TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI, FEBRUARI 2019


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS - TAMISEMI











TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA ZA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI, FEBRUARI 2019


Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuutangazia Umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli, anaendelea na kuongeza idadi ya watumishi katika Sekta ya Umma kwa kutoa nafasi nyingine za ajira kwa vijana wa Kitanzania katika Sekta ya Elimu. Mchakato huu wa sasa wa ajira utahusisha ajira mpya za watumishi 4549. Ajira hizi zitahusisha walimu wa Shule za Msingi na Sekondari.


Kwa sababu hiyo, OR-TAMISEMI inawatangazia walimu wenye sifa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha http://ajira.tamisemi.go.tz (Online Teacher Employment Application System OTEAS).


Walimu wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

A.              WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA MSINGI

i.          Mwalimu Daraja la IIIA - mwenye Astashahada (Cheti) ya Ualimu;

ii.     Mwalimu  Daraja  la  IIIB  -  mwenye  Stashahada  (Diploma  ya  Ualimu  katika







2


masomo ya English, Civics, Historia, Jiografia na Kiswahili;

B.           WALIMU WATAKAOAJIRIWA SHULE ZA SEKONDARI

i.               Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;

ii.            Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum;

iii.         Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics , Biology & Chemistry;

iv.         Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Agriculture Science;
v.            Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Home Economics;

vi.         Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Physics, Mathematics, Chemistry & Biology;

vii.         Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la Book Keeping, Commerce, Accounts & Economics; na
viii.             Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu somo la English, Civics

&  General Studies.




ix.                   Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Mahitaji Maalum aliyehitimu Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.



x.            Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu kwa masomo ya English, Civics, General Studies, History, Geography & Kiswahili.






3






C.              SIFA ZA JUMLA

Waombaji wa nafasi tajwa hapo juu wawe na sifa za jumla zifuatazo:-

i.            Awe ni Mtanzania;

ii.          Awe amehitimu chuo kinachotambulika na Serikali kati ya mwaka 2014 hadi 2017; isipokuwa kwa wahitimu wa Elimu ya Ualimu wa masomo ya Fizikia na

Hisabati;

iii.            Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45) wakati wa kutuma maombi haya;

iv.            Walimu waliowahi kutuma maombi na hawajaajiriwa wanapaswa kutuma maombi upya.


D.              MWISHO

Maombi yote yawasilishwe kwa mtandao na yawe na nakala za vyeti vya taaluma,utaalam na kuzaliwa. Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 15/03/2019.




















4

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.