Skip to main content

Kizunguzungu

 


Tatizo La Kusikia Kizunguzungu – Vertigo

 

kizunguzungu

 

Ukiwa mdogo, ulishashiriki mchezo ambapo ulijizungusha au ulipanda kwenye ule mchezo wa kuzunguka (merry-go-round)? Kama ulifanya michezo hiyo, utakumbuka hali iliyokupata baada ya mchezo. Dunia yote ilizunguka mbele yako. Kuna tatizo ambalo humpata mtu, akiwa umesimama kidete akahisi dunia yote inazunguka. Tatizo hili kitaalamu huitwa vertigo. Kitaalamu, tatizo hili linahusishwa na dosari za ndani ya maeneo ya mwili ya kutuwezesha kusimama bila kuyumba, yaliyomo ndani ya sikio na kwenye ubongo. Vertigo ni hali ya kuona kuwa chumba na mazingira yanayokuzunguka, vyote vikiwa kwenye duara, kukuzunguka wewe. Kwa lugha ya kawaida, ni tatizo la kusikia kizunguzungu.

Vertigo inaweza kutokea kama mtu atachungulia chini kutoka sehemu iliyo juu sana, lakini mara nyingi tunamaanisha hali inayotokea kwa muda mfupi au kizunguzungu cha muda mrefu kutokana na dosari za sehemu ya ndani ya sikio au ubongo.

Vertigo si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuleta kizunguzungu.

Ili kulifahamu tatizo la vertigo, ni vizuri kuufahamu muundo wa sikio. Mawimbi ya sauti yanasafiri na kuingia ndani ya sikio hadi yanapofika kwenye eardrum. Kuanzia pale sauti hubadilishwa na kuwa mtingishiko ambao huingia sehemu ya kati ya sikio kupitia mifupa midogo mitatu –incus, malleus na stapes — kwenda kwenye cochlea na hatimaye kwenda hadi kwenye vestibular nerve ambaye husafirisha taarifa hiyo kwenye ubongo ambao hutafsiri ishara hizo kama sauti.

 

muundo wa sikio

Sehemu ya ndani ya sikio haihusiki na kusikia. Hujengwa na maumbo madogo ya nusu mviringo matatu (vestibular labyrinth), kila moja likiwa pembe mraba kutoka jingine, yenye majimaji na sensor ndogo mithili ya nywele zinazofuatilia mizunguko ya kichwa.

Maumbile mengine (otolith organs) ndani ya sikio hufuatilia miondoko ya kichwa chako – juu na chini, kulia na kushoto, nyuma na mbele – na kichwa chako kilipo kutoka kwenye mvutano wa dunia. Viungo hivi vya otolith vina chembechembe zinazokuwezesha kuhisi nguvu ya mvutano wa dunia.

Kwa sababu mbalimbali, chembechembe huweza kutoka kwenye sehemu zake. Zikitoka , zinaweza kuingia kwenye moja ya maumbo haya ya mviringo – na hasa ukiwa umelala chini. Hali hii husababisha maumbo ya mviringo kuhisi mabadiliko ya mkao wa kichwa ambayo haingeyafuatilia, na utapata kizunguzungu.

 

Dalili za Vertigo

 

Mtu mwenye vertigo husikia kama kichwa chake au nafasi inayomzunguka inazunguka.

Vertigo ni dalili, lakini inaweza kusababisha au kutokea pamoja na dalili nyingine.

Zikiwa ni pamoja na:

. Matatizo ya kuyumba
. Kujisikia mwepesi
. kichefuchefu au kutapika
. sauti ndani ya masikio (tinnitus)
. Kuona kama sikio limejaa
. maumivu ya kichwa
. macho kucheza kutoka upande mmoja hadi mwingine (nystagmus)

 

Chanzo Cha Vertigo

 

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha vertigo, mara nyingi vikihusiana na matatizo ya ndani ya sehemu ya ndani ya sikio au katika ubongo (central nervous system).

Mazingira yanayoweza kuleta vertigo ni pamoja na:

 

Labyrinthitis

Tatizo hili linaweza kutokea pale maambukizi yatakaposababisha uvimbe kwenye sehemu ya ndani ya labyrinth. Ndani ya labyrinth kuna neva (vestibulocochlear verve).

Neva hii hupeleka taarifa kwenye kichwa kuhusu miondoko, mkao wa kichwa na sauti.

Mtu mwenye maambukizi kwenye labyrinth anaweza kupoteza uwezo wa kusikia, mivumo masikioni (tinnitus), maumivu ya kichwa, maumivu ya masikio, na kutoona vizuri.

 

sikio

 

 

Vestibular neuritis

Maambukizi husababisha vestibular neuritis, uvimbe kwenye vestibular nerve. Ni hali inayofanana na labyrinthitis lakini haiathiri uwezo wa kusikia. Vestibular neuritis husababisha kizunguzungu ambacho huweza kuambatana na kuona kwa ukungu, kichefuchefu kikubwa, na kujisikia unayumba.

 

Cholesteatoma

Hii ni ngozi isiyo ya kansa inayoota sehemu ya katikati ya sikio, mara nyingi baada ya maambukizi ya kujirudia. Kadiri inavyoota nyuma ya eardrum, inaweza kuharibu muundo wa sehemu ya kati yenye mifupa, na kusababisha kushidwa kusikia au kizunguzungu.

 

Ménière’s disease

Ugonjwa huu husababisha kuongezeka kwa majimaji ndani ya sehemu ya ndani ya sikio, na huweza kusababisha vipindi vya kushikwa na kizunguzungu vinavyoambatana na mvumo kwenye masikio na kupoteza uwezo wa kusikia. Ugonjwa huu huonekana sana baina ya watu wa umri wa kati ya miaka 40 na 60.

Sababu kamili ya ugonjwa huu haieleweki, lakini pengine inatokana na kusinyaa kwa mishipa ya damu, maambukizi ya kirusi, au ugonjwa unaotokana na kinga za mwili (autoimmune reaction). Laweza kuwa tatizo la kiurithi.

Benign paroxysmal positional vertigo (BPPV)

Sehemu ya ndani ya sikio ina viungo viitwavyo otolith, ambavyo ndani yake vina majimaji na chembechembe za calcium carbonate.

BPPV ni hali ambapo chembechembe hizi hutoka kwenye sehemu yake na kuingia kwenye semicircular canals. Zikiwa pale, kila chembechembe hugusa seli za ufahamu zilizo kama vinywelea ndani ya cupula wakati wa kutembea.

Mapato yake, ubongo hupata taarifa ya uwongo kuhusu mtu alivyokaa, na kizunguzungu hutokea. Watu hupata vipindi vya kizunguzungu ambavyo havizidi sekunde 60, lakini kichefuchefu na dalili nyingine pia vyaweza kutokea.

Sababu nyingine

Kizunguzungu kinaweza kutokea pia kwa sababu zifuatazo:

. kipandauso
. kuumia kichwani
. upasuaji wa sikio
. perilymphatic fistula, ambapo majimaji kutoka sehemu ya ndani ya sikio yanavujia kwenye sehemu ya kati ya sikio kwa sababu ya kupasuka kwa moja ya ngozi mbili nyembamba zinazotenganisha eneo la kati na eneo la ndani la sikio
. mkanda wa jeshi kuzunguka sikio
. otosclerosis, wakati mfupa wa sehemu ya kati ya sikio unapokuwa na tatizo la ukuaji ambalo linasababisha kutosikia
. kaswende
. kiharusi
. acoustic neuroma, ambao ni uvimbe unaoota juu ya vestibulocochlear nerve karibu na sehemu ya ndani ya sikio
. multiple sclerosis

Kulala kitandani kwa muda mrefu na matumizi ya baadhi ya madawa pia huleta vertigo.

Kizunguzungu na ujauzito

Kichefuchefu na kizunguzungu ni matatizo ya kawaida wakati wa ujauzito. Mabadiliko ya homoni yanaonekana kuwa sababu, kwa sababu huathiri tabia ya majimaji ndani ya mwili.

 

Tiba Ya Vertigo

 

Tiba inaweza kutolewa kulingana na aina ya tatizo. Daktari anaweza kukuandikia antibiotics au antiviral drugs kwa ajili ya mkanda wa jeshi.

Upasuaji unaweza kuwa wa lazima kama tiba nyingine hazikutoa mafanikio.

 

Tiba ya mimea

Baadhi ya mimea inaweza kusaidia kuondoa tatizo. Nayo ni pamoja na:

. cayenne
. tumeric
. ginkgo biloba
. ginger root
. Gongjin-dan

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.