Liverpool yatinga nusu Fainali
Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Furaha ya ushindi ya wana Liverpool Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10 baada ya kujikokota na kuishinda Manchester City kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 yaliyoleta ushindi wa jumla wa Liverpool 5-1 Man City. City walianza vizuri wakati walipojaribu kulipa deni la 3-0 walizofungwa katika mechi ya kwanza. Ilikuwa dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Raheem Sterling alimwanzishia Gabriel Jesus aliyeitumia nafasi hiyo kupachika bao la kuwapa matumaini Man City. Hata hivyo baada ya tukio la vurugu kabla ya muda wa mapumziko lililoisha kwa Meneja Pep Guardiola kuondoshwa katika eneo la benchi la ufundi, City hawakuweza kuyafikia matamanio yao. Tukio lenyewe lilianzia pale ambapo Bernardo Silva alikuwa amepiga mkwaju kuelekea lango la Liverpool, huku Liverpool ikiwa katika shinikizo zito, mpira ukamkuta Leroy Sane ambaye aliukwamisha wavuni na kuwafanya City kudhani wamefanikiwa kupata goli la ...