Liverpool yatinga nusu Fainali

SportsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFuraha ya ushindi ya wana Liverpool
Liverpool imefika katika nusu fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa miaka 10 baada ya kujikokota na kuishinda Manchester City kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 yaliyoleta ushindi wa jumla wa Liverpool 5-1 Man City.
City walianza vizuri wakati walipojaribu kulipa deni la 3-0 walizofungwa katika mechi ya kwanza. Ilikuwa dakika ya pili tu ya mchezo ambapo Raheem Sterling alimwanzishia Gabriel Jesus aliyeitumia nafasi hiyo kupachika bao la kuwapa matumaini Man City. Hata hivyo baada ya tukio la vurugu kabla ya muda wa mapumziko lililoisha kwa Meneja Pep Guardiola kuondoshwa katika eneo la benchi la ufundi, City hawakuweza kuyafikia matamanio yao.
Tukio lenyewe lilianzia pale ambapo Bernardo Silva alikuwa amepiga mkwaju kuelekea lango la Liverpool, huku Liverpool ikiwa katika shinikizo zito, mpira ukamkuta Leroy Sane ambaye aliukwamisha wavuni na kuwafanya City kudhani wamefanikiwa kupata goli la pili.
Lakini hali ilikuwa tofauti kwani mwamuzi Antonio Mateu Lahoz alilikataa goli hilo kwa madai kuwa limepatikana katika mazingira ya kuotea yaani offside, jambo ambalo limemkera Pep Guadiola aliyeingia uwanjani kumkabili mwamuzi Antonio Mateu Lahoz, na hivyo meneja huyo wa City kuambulia kufukuzwa katika eneo lake la ufundi hali iliyomfanya kulazimika kuitizama kipindi cha pli akiwa katika viti vya mashabiki.
City wakijaribu kupambana katika mazingira ambayo mwalimu wao yuko mbali, wakapoteza mwamko na kuwapa nafasi wageni Liverpool kupitia Mohamed Salah akajipatia bao lake la 39 la msimu baada ya mbio za nguvu kutoka kwa Sadio Mane mnamo dakika ya 56.
Goli zuri la Robert Firmino dakika 13 kabla ya kumalizika kwa mchezo, limekuwa msumali wa mwisho katika jeneza la Man City na hivyo kuwahakikishia Liverpool kusonga mbele.
Sasa Liverpool wanasubiri kuwajua wapinzani wao katika nusu fainali wakati droo itakapochezeshwa Ijumaa [12:00 BST] huko Nyon, Uswisi.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU