Mambo 6 ya kutegemea Zuckerberg atakapotoa ushahidi kwa mabaraza ya Congress

Mark Zuckerberg Mkurigenzi Mkuu wa kampuni ya FacebookHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBwana Zuckerberg atakabiliana na hoja kali kuoka kwa mabunge yote mawili ya Marekani kuhusu taarifa/ data za kibinafsi hususan zile zinazolenga sakata la Cambridge Analytica
Mark Zuckerberg amekuwa akijiandaa kwa jaribio lake kubwa huku Mkurugenzi mkuu huyo wa Facebook - akikabiliwa na maswali kutoka kwa mabaraza yote mawili ya congress
Baadhi wanaonelea vikao hivi viwili kama zaidi ya mchezo wa kisiasa wa kuigiza , kama ni fursa ya wanasiasa kuonekana kwente Ttelevisheni wakimkosoa kwa ukali mtu tajiri na mwenye mamlaka.
Huenda kukawa na ukweli katika hili. Lakini ni dhahiri kwamba haijawahi kutokea nafasi ya kumchambua Zuckerberg ambaye hapatikani kwa urahisi kutokana na kulindwa na kufichwa na kikosi chake cha maafisa wa mahusiano ya ummapamoja na manaibu wake.
Taarifa yake ya ufunguzi wa iliyoandaliwa tayari imetolewa.
Lakini vikao hivyo vya mabunge mawili vilivyopangwa kufanyika Jumanne na Jumatanmo Wednesday vitakwenda mbali zaidi.
Bwana Zuckerberg atakabiliana na hoja kali kuhusu taarifa/ data za kibinafsi - hususan zile zinazolenga sakata la Cambridge Analytica - na ni kwa vipi gazeti ndilo lililoweza kugundua uingiliwaji wa mifumo yake.
Na atatarajia baadhi ya maswali magumu juu ya uingiliaji wa uchaguzi wa Marekani na hali ya usoni ya mtandao wake wa kijamii wa Facebook.
Mambo ya kuangalia wakati Bw Zuckerberg akielekea kwenye mabunge ya Congress ya Marekani:

1. Kuangaziwa kwa mema

Jamii , jamii, jamii. Ni neno utakalokuwa ukilisikia sana kutoka kwa Bw Zuckerberg ambaye atafungua kauli zake kwa kusisitizia mazuri ambayo Facebook inayaleta duniani.
Na yuko sahihi. Imeyafanya maisha yetu halisi kuwa kuwa ya bora zaidi , iwe maandalizi ya sherehe ya siku ya kuzaliwa ama maandamano ya upinzani , vimekuwa sana kutokana na Facebook. Kutokana na kwamba unaweza kuwashirikisha wana familia na marafiki picha.
Atazungumzia kuhusu namna Facebook inatumiwa na wafanyabiashara wadogo kote duniani kuwafikia wateja wao haraka, kwa usahihi na kwa gharama ya chini.
Kwa njia iliyo ya moja kwa moja atakuwa alisema msiihukumu sana biashara yangu, kwasababu kwa kufanya hivyo mnaweza kuwaathiri mamilioni ya watu wenginepia.

2. Atajaribu kuonyesha kuwa mambo ni ya kawaida

Kwa Zuckerberg mwenye umri wa miaka 33 , ambaye anaelewa namna kampuni yake inavyofanya kazi hatakuwa tatizo .Si Mkurugenzi Mkuu anayejificha tu kwenye kumbi za mikutano ya bodi, ana uelewa zaidi kuhusu kampuni yake.
Pia anaweza pia kuelezea masuala ya ndani ya kiufundi ya kamuni yake.
Badala yake , changamoto kwake itakuwa ni kuonekana kwa ubinadamu wake na kukabiliana na majuto - hata kama yeye binafsi moyoni mwake bado anaamini kwamba , kama kampuni ilivyosema awali, watumiaji hao walitoa data/taarifa zao kwa utashi wao.

3. Atamlaumu Kogan

Ni muhimu kukumbuka kwamba wakati Facebook imekiri makosa kuhusina na sera ya taarifa/data na namna ilivyokuwa ikifanya mambo yake kwa usahihi (ama kutokuwa sahini ) katika kujitakasa kwa makosa ya awali , kampuni hiyo imeshikilia kuwa ni Aleksandr Kogan, mtafiti katika chuo kikuu cha Cambridge , mwenye makosa kw akiasi kikubwa.
Ni Bw Kogan ambaye alibuni programu binafsi ambayo ilikukusanya data ambazo baadae zilidaiwa kutumiwa na Cambridge Analytica . Na ilikuwa Cambridge Analytica ambayo ilisema ilifuta data wakati haikufanya hivyo.
Bw Zuckerberg atajaribu kuonyesha kuwa ni jambo zuri kuhakikisha kuwa wanasiasa wanafahamu mifumo ya Facebook, huku pia akijaribu kutoonekana kana kwamba anawaeleza kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao.
Mark ZuckerbergHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMark Zuckerberg atavalia nembo yake fulana ya rangi ya kijivu wakati atakaposikilizwa na mabunge ya Marekani

4. Atawahusisha kampuni nyingine

Kwa wakati mmoja kabla ya kusikilizwa kwao , wabunge walitaka wakuu wa kampuni ya Google na Twitter wahojiwe sambamba na Zuckerberg - wakibainisha kuwa maswali mengi yanayowakabili yanawahusu wote.
Kulikuwa na propaganda nyingi za Urusi kwenye Twitter kwa mfano , na mvutano wa YouTube ambao uliorekodiwa na kuhifadhiwa vema.
Hilo halitafanyika sasa. Facebook iko peke yake. Lakini hilo halitamzuwia Bw Zuckerberg kujaribu kuyavuta makampuni mengine ya teknolojia katika mjadala huu, hata kama hatayataja majina
Facebook haikuwa kampuni ya kwanza kutengeneza mabilioni ya dola kutokana na data binafsi na haitakuwa ya mwisho.

5. Majigambo ya kisiasa na maswali mabaya

''Ni Maswali yenye majibu rahisi ya ndio au hapana ," ni maswali yanaopendwa na wanasiasa katika vikao vya aina hii. Yanafaa zaidi hasa ,pale unapouliza swali ambalo majibu yake ni huwa ni ndio au hapana.
Tarajia kamera kuwaangazia wawakilishi wakati wa kikao hicho, kuwapata wabunge wenye ushawishi zaidi wakiuliza maswali kwa ajili ya kuandaa video za kuwanadi kabla ya kura za nuru ya muhula.
Tarajia bila shaka mmmoja wa wabunge kuuliza '' unaweza kuapa hapa leo kwamba Facebook haitauza data za watumiaji? " - swali ambalo jibu lake litakuwa "bila shaka ". Facebook haijawahi kamwe kuuza data, haitoi kabisa uwezo wa kuzifukia.
Nembo ya FacebookHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBw Zuckerberg mwenye umri wa miaka 33 atakabiliwa na changamoto ya kuonekana kwa ubinadamu wake na kukabiliana na majuto

6. Mazungumzo yasiyo na mjadala juu ya sheria

Bw Zuckerberg ataelezea kuhusu kipengele kinachoonyesha ukweli juu ya matangazo ya kibiashara - muswada wa sheria ambao utaongeza zaidi uwazi katika matangazo ya kujinadi kwa wanasiasa kwenye mtandao.
Mazungumzo haya yatawarejesha wabunge zaidi kwenye kile kinachoendelea kwenye televisheni , ambako iliwekwa wazi kuhusu nani aliyelipia tangazo la biashara.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU