VYAKULA VYA KUPAMBANA NA MARADHI YA MAFUA
Mafua ni ugonjwa unaosumbua watu kila mwaka, hasa yanayo anza kutokea mabadiliko ya hali ya hewa kutoka msimu wa kiangazi kuingia masika.
Ili kujikinga na ugonjwa wa mafua ni lazima mwili uwe na kinga ya kutosha.
Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi kikubwa cha protini na virutubisho vingine.
SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa na virutubisho vinavyo saidia kupunguza utokaji wa makamasi.
Supu ya kuku |
Utapata virutubisho vingi zaidi ukitengeneza supu ya kuku kwa kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.
VITUNGUU SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya ‘ allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magojwa mbalimbali ya kuambukiza.
Vitunguu Saumu |
Kitunguu saumu kinatoa kinga halikadhalika kinapunguza muda wa mtu kuumwa na mafua.
Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje.
CHAI
Chai hasa ya kijani, ( Green Tea ) ina virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili .
Chai Ya Kijani |
Utafiti wa hivi karibuni ulio fanywa na jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani ( Journal Of the American College of Nutrition ) umeonyesha kuwa watu wanao tumia chai kwa mpangilio maalumu, hawasumbuliwi mara kwa mara na mafua pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza, huwa salama na mafua au siku za kuumwa mafua hupungua kwa asilimia 36 ukilinganisha na wale wasio kuwa na kinga imara.
Hata hivyo, tahadhari inatolewa kwa watoto wa shule kutokupewa kiasi kingi cha chai kwa siku.
Unywaji wa kikombe kimoja kwa siku kwa motto wa shule siyo mbaya.
Kwa mtu mzima, usizidishe vikombe vitatu kwa siku.
Ikumbukwe kuwa, chai inapotumika kwa wingi kupita kiasi, huweza kusababisha pia tatizo la kukosa choo kwa muda mrefu.
Kunywa kiasi kwa afya yako.
MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonyesha kwamba, ulaji wa vyakula vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa mafua.
Machungwa |
Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C ni pamoja na machungwa, mboga za majani aina ya Brokoli na pilipili kali.
Pilipili Kali |
Ili kupata kiasi kingi cha Vitamin C, inashauriwa machungwa yaliwe pamoja na nyama zake za ndani au kunywa juisi yake.
ASALI
Kama inavyo julikana, asali ni tiba ya matatizo mengi ya kiafya, miongoni mwa hayo ni pamoja na mafua.
Asali inasaidia kuondoa kikohozi na muwasho kwenye koo. Halikadhalika, asali inaweza kutumiwa na watoto wadogo kama dawa.
Watoto wanao ruhusiwa kutumia asali kama tiba ni wa umri wa kati ya miaka 2 hadi 5.
Hawa dozi yao ni nusu kijiko kidogo cha asali, wenye umri wa miaka 6 hadi 11 wapewe kijiko kimoja kidogo na wenye umri wa kuanzia miaka 12 hadi 18, wapewe vijiko vidogo viwili vya asali wakati wa kulala.
MTINDI
Kutokana na kiwango kikubwa cha protini ilicho nacho, Mtindi ni chakula kingine kinachofaa kuliwa na mtu mwenye mafua ili kupunguza siku za kusumbuliwa na ugonjwa wa kukohoa.
Wataalamu wanakubaliana kuwa, ulaji wa ‘chocolate’ nyeusi ( Dark Chocolate ), huimarisha kinga ya mwili, hivyo inapoliwa na mgonjwa wa mafua, huweza kumpa ahueni mgonjwa kwa namna moja ama nyingine, na pia huwa kinga kwa magonjwa mengine.
PWEZA
Samaki aina ya pweza wana virutubisho vingi vya kuongeza kinga ya mwili yenye uwezo wa kupambana na bacteria pamoja na virusi vya mafua.
Kiasi kidogo cha pweza, awe wa kukaangwa au kuchemshwa kama supu, anafaa kuliwa mara kwa mara kukmarisha kinga ya mwili.
VIAZI VITAMU
Kirutubisho hicho huwa ni muhimu kwa ustawi na uimarishaji wa kinga mwilini na kinapatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu na vyakula vingine kama vile karoti, maboga na mayai ( kiini)
Kwa ujumla , suala la kuimarisha kinga ya mwili ni muhimu kwa afya zetu.
Comments
Post a Comment