Wengi tumekuwa tukitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga lakini wachache mno wanaojua faida za nyanya chungu kiafya. Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha afya ya mlaji. Nyanya chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi ikiwemo vitamin A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuobresha afya ya mwili kwa ujumla. Nyanya chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na magonjwa ya mara kwa mara. Hizi pia ni kinga iayoweza kumwepusha mlaji kupata maradhi ya moyo. Kwa wagonjwa wa kisukari nyanya chungu pia ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza kiwango cha sukari ndani ya mwili. Vitamin K inayopatikana ndani ya nyanya chungu inasaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu. Licha ya kuwa karibu asilimia ...
NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu, ambavyo ni kitambulisho cha raia, kitambulisho cha mgeni mkaazi, na kitambulisho cha mkimbizi. Mahitaji yake: Cheti cha kuzaliwa Cheti za elimu ya msingi, Pasi ya kusafiria ( Pasipoti ) Cheti cha elimu ya sekondari ( kidato cha iv na vi ) leseni ya udereva Kadi ya bima ya afya Kadi ya mfuko wa hifadhi ya jamii Kadi ya mpiga kura Nambari ya mlipa kodi ( Tin. No ) Kitambulisho cha mzanzibar mkazi Barua kutoka kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa CLICK HERE https://services.nida.go.tz/nidportal/NID_Copy.aspx
Tatizo La Kusikia Kizunguzungu – Vertigo Ukiwa mdogo, ulishashiriki mchezo ambapo ulijizungusha au ulipanda kwenye ule mchezo wa kuzunguka (merry-go-round)? Kama ulifanya michezo hiyo, utakumbuka hali iliyokupata baada ya mchezo. Dunia yote ilizunguka mbele yako. Kuna tatizo ambalo humpata mtu, akiwa umesimama kidete akahisi dunia yote inazunguka. Tatizo hili kitaalamu huitwa vertigo. Kitaalamu, tatizo hili linahusishwa na dosari za ndani ya maeneo ya mwili ya kutuwezesha kusimama bila kuyumba, yaliyomo ndani ya sikio na kwenye ubongo. Vertigo ni hali ya kuona kuwa chumba na mazingira yanayokuzunguka, vyote vikiwa kwenye duara, kukuzunguka wewe. Kwa lugha ya kawaida, ni tatizo la kusikia kizunguzungu. Vertigo inaweza kutokea kama mtu atachungulia chini kutoka sehemu iliyo juu sana, lakini mara nyingi tunamaanisha hali inayotokea kwa muda mfupi au kizunguzungu cha muda mrefu kutokana na dosari za sehemu ya ndani ya sikio au ubongo. Vertigo si ugonjwa bali ni dalili y...
Comments
Post a Comment