TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA WIZARA YA AFYA
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb Na. FA 97/128/01/”A’’/31 cha tarehe 12 Julai 2019 kwa ajili ya kuajiri watumishi 550 wa kada mbalimbali za afya. Hivyo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inapenda kuwatangazia wahitimu wote wa kada za Afya nchini kuwasilisha maombi ya nafasi za kazi, kuanzia leo tarehe 22/07/2019 ili kujaza nafasi mbalimbali za Kada ya Afya katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati. Nafasi zinazotangazwa ni zifuatazo:- 1. Daktari Daraja la II Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika). 2. Tabibu Daraja la II Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Utabibu ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. 3. Tabibu Msaidizi Wao...