TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA WIZARA YA AFYA
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) imepata
kibali cha ajira mbadala chenye Kumb Na. FA 97/128/01/”A’’/31 cha tarehe
12 Julai 2019 kwa ajili ya kuajiri watumishi 550 wa kada mbalimbali za afya.
Hivyo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI inapenda kuwatangazia wahitimu wote wa
kada za Afya nchini kuwasilisha maombi ya nafasi za kazi, kuanzia leo tarehe
22/07/2019 ili kujaza nafasi mbalimbali za Kada ya Afya katika Hospitali za
Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.
Nafasi zinazotangazwa ni zifuatazo:-
1. Daktari Daraja la II
Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo
Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi
“Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka
Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
2. Tabibu Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Utabibu ya muda wa miaka
mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
3. Tabibu Msaidizi
Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili ya Tabibu
Wasaidizi (Clinical Assistants Certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa
na Serikali.
4. Afisa Muuguzi Daraja la II
Waombaji wawe na Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini
(Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na
Wakunga Tanzania.
5. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi ya muda
usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali,
waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
6. Muuguzi Daraja la II
Waombaji wawe na Cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika
Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa (Enrolled) na Baraza la
Wauguzi na Wakunga Tanzania.
7. Afisa Afya Mazingira Daraja la II
Waombaji wawe na Shahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira na mafunzo
kazini na kusajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Afya ya Mazingira.
8. Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka
mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Bodi ya
Wataalam wa Afya Mazingira.
9. Mteknolojia Daraja la II (Maabara)
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Sayansi ya Maabara ya
muda wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na
kusajiliwa na Mabaraza ya Taaluma.
10.Mteknolojia Msaidizi (Maabara)
Waombaji wawe wamehitimu Astashahada ya miaka miwili katika fani ya
Maabara kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao
wamesajiliwa na Mabaraza yao pale inapohusika.
11.Mteknolojia Daraja la II (Mionzi)
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Sayansi ya Mionzi ya muda
wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa
na Mabaraza ya Taaluma.
12.Mteknolojia Daraja la II (Dawa)
Waombaji wawe na Stashahada (Diploma) ya Sayansi ya Dawa ya muda
wa miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa
na Mabaraza ya Taaluma.
13.Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II
Waombaji wawe na Stashahada ya miaka mitatu (Diploma) katika fani ya
Fiziotherapia/ Mtoa Tiba kwa Vitendo kutoka Chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
14.Msaidizi wa Afya (Mhudumu wa Afya)
Waombaji wawe wahitimu wa kidato cha nne waliopata mafunzo ya
Mwaka mmoja katika fani ya afya katika chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
SIFA ZA MWOMBAJI;
i. Awe raia wa Tanzania;
ii. Awe na umri usiozidi miaka 45;
iii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au asiwe Mwajiriwa wa Hospitali za
Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwa na Serikali;
iv. Asiwe amewahi kuajiriwa Serikalini;
v. Asiwe na check namba, na endapo itabainika kuwa aliwahi kuajiriwa
Serikalini, atatakiwa kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika
Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye
Waraka Na. CCB 228/271/01 wa tarehe 07 Agost, 2012.
MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA;
i. Nakala ya cheti cha kidato cha nne/sita;
ii. Nakala za Vyeti vya Taaluma;
iii. Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
iv. Nakala ya cheti cha usajili kamili (Full Registration) au Leseni ya
kufanya kazi ya taaluma husika;
4
v. Maelezo binafsi (CV); na
vi. Waombaji wanaojitolea na wale wanaomaliza muda wa ajira za
mikataba kutoka kwa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Afya
wanatakiwa kuambatanisha barua za uthibitisho kutoka kwa
Wakurugenzi wa Halmashauri husika.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI WOTE
i. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi Halmashauri yoyote
watakayopangiwa;
ii. Waombaji wote wawe tayari kufanya kazi na mashirika/taasisi
zilizoingia ubia na Serikali;
iii. Waombaji waliosoma nje ya nchi wanatakiwa waambatanishe pamoja
na equivalent certificate kutoka NECTA/NACTE/TCU; na
iv. Waombaji watakaotuma/waliotuma maombi yao ya kazi Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto hawapaswi
kuomba nafasi hizi za kazi za Ofisi ya Rais, TAMISEMI.
Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa
kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ya ajira.tamisemi.go.tz.
Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa
moja Ofisini hayatafanyiwa kazi.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 05 Agosti, 2019 saa 9:30 alasiri.
Tangazo hili linapatikana katika tovuti yetu
www.tamisemi.go.tz
Limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais - TAMISEMI,
Mji wa Serikali – Mtumba,
S.L.P 1923,
DODOMA.
22 Julai, 2019
Click here to start application
http://ajira.tamisemi.go.tz
http://ajira.tamisemi.go.tz
Comments
Post a Comment