Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 24.03.2018
Image caption Neymar huenda akaikosa michuano ya kombe la dunia kwa kuwa majeruhi Manchester City na Manchester United zote kwa pamoja zitapambana kujaribu kumsajili nyota wa Brazil Neymar iwapo ataamua kuondoka Paris St-Germain. Real Madrid pia wanajaribu kupata saini yake, lakini PSG wamesema hawamuachii. (Mundo Deportivo - in Spanish) Kufuatia kocha wa Manchester Jose Mourinho kumshambulia kwa maneno mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Luke Shaw, kunaweka pia hatarini kumpata winga wa Real Madrid na raia wa Wales Gareth Bale. (mail) Gareth Bale ataondoka Real Madrid na kujiunga na Manchester United wakati wa majira ya joto iwapo Zinedine Zidane atasalia kuiongoza miamba hiyo ya Bernabeu .(mirror) Lakini mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ameambiwa na meneja wa Wales na kiungo wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs kusalia katika La Liga kuliko kurudi Premier League. (express) Image caption Rashford ataiongoza Uingereza kwenye safu ya ushambuliaji katika michuano ya kombe la ...