Umoja na amani ya Tanzania viko hatarini;Maaskofu wa kilutheri waonya

Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatariniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBaraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) limetoa waraka maalum wa Pasaka
Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) linasema umoja na amani ya Tanzania viko hatarini.
Katika waraka wa ujumbe wa pasaka unaosambaa katika mitandao ya kijamii na kutarajiwa kusomwa kesho katika makanisa mbali mbali ya KKKT nchini Tanzania, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.
Waraka umeyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji
yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.
"Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na
kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na
ubabe, vurugu, hila, na vitisho", imesomeka sehemu ya waraka huo
Waraka umeongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.
Ujumbe huu kutoka baraza la maaskofu wa KKKT umekuja siku chache tu baada ya ujumbe wa Kwaresima uliotolewa na baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki
"Shughuli za kisiasa kama vile maandamano, mikutano ya hadhara, ambayo ni haki ya kila raia, vinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola", inasomeka sehemu ya waraka huo wa Maaskofu wa kanisa Katoliki
Maaskofu wa Katoliki waligusia pia kuminywa kwa uhuru wa kutoa na kupokea habari huku wakitaja baadhi ya vyombo vya habari kufungiwa au kusimamishwa kwa muda.
Walionya kwamba katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu.
Maaskofu wa KKKT wameasa kwamba roho iliyokuwemo kwa waasisi wa taifa na hata kusaidia kupata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu, inapaswa kuendelea wakati wote
"Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru na Umoja ndizo ngao zetu
zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50", wamesema maaskofu wa KKKT

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)