Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 24.03.2018

Neymar huenda akaikosa michuano ya kombe la dunia kwa kuwa majeruhi
Image captionNeymar huenda akaikosa michuano ya kombe la dunia kwa kuwa majeruhi
Manchester City na Manchester United zote kwa pamoja zitapambana kujaribu kumsajili nyota wa Brazil Neymar iwapo ataamua kuondoka Paris St-Germain.
Real Madrid pia wanajaribu kupata saini yake, lakini PSG wamesema hawamuachii. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kufuatia kocha wa Manchester Jose Mourinho kumshambulia kwa maneno mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Luke Shaw, kunaweka pia hatarini kumpata winga wa Real Madrid na raia wa Wales Gareth Bale. (mail)
Gareth Bale ataondoka Real Madrid na kujiunga na Manchester United wakati wa majira ya joto iwapo Zinedine Zidane atasalia kuiongoza miamba hiyo ya Bernabeu .(mirror)
Lakini mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ameambiwa na meneja wa Wales na kiungo wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs kusalia katika La Liga kuliko kurudi Premier League. (express)
Rashford ataiongoza Uingereza kwenye safu ya ushambuliaji katika michuano ya kombe la dunia mwaka huu
Image captionRashford ataiongoza Uingereza kwenye safu ya ushambuliaji katika michuano ya kombe la dunia mwaka huu
Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 20, ameibuka kuwa gumzo kwa klabu ya Real Madrid wakihitaji kumsajili majira ya joto. (Sport via Mail)
Vilabu vya Manchester City na Manchester United vinawania kumsajili mlinzi wa kati wa Ujerumani na Bayern Munich Jerome Boateng. (Sun)
Meneja wa Ubelgiji Roberto Martinez haamini kutumiwa kwa kiungo Eden Hazard kama mshambuliaji wa kati, na anaamini kocha Antonio Conte anamtumia visivyo mchezaji huyo. (Express)
Miongoni mwa vilabu vinavyomuania Sessegnon ni pamoja na United na Tottenham
Image captionMiongoni mwa vilabu vinavyomuania Sessegnon ni pamoja na United na Tottenham
Kiungo wa Fulham Ryan Sessegnon hataihama timu hiyo iwapo itafuzu kushiriki michuano ya ligi kuu msimu ujao.(Sun)
Mshambuliaji wa West Ham Manuel Lanzini, amekanusha kuihama klabu hiyo na kusema anafurahia maisha katika jiji la London. (West Ham website)
Manchester United imetenga kitita cha Pauni milioni 40 kumshajili kiungo wa Bayern Munich na Brazil Douglas Costa, aliye kwa mkopo Juventus. (Mirror)

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.

UWEZO WA AJABU WA JUISI YA KITUNGUU