Posts

Showing posts from November, 2021

Kizunguzungu

Image
  Tatizo La Kusikia Kizunguzungu – Vertigo     Ukiwa mdogo, ulishashiriki mchezo ambapo ulijizungusha au ulipanda kwenye ule mchezo wa kuzunguka (merry-go-round)? Kama ulifanya michezo hiyo, utakumbuka hali iliyokupata baada ya mchezo. Dunia yote ilizunguka mbele yako. Kuna tatizo ambalo humpata mtu, akiwa umesimama kidete akahisi dunia yote inazunguka. Tatizo hili kitaalamu huitwa vertigo. Kitaalamu, tatizo hili linahusishwa na dosari za ndani ya maeneo ya mwili ya kutuwezesha kusimama bila kuyumba, yaliyomo ndani ya sikio na kwenye ubongo. Vertigo ni hali ya kuona kuwa chumba na mazingira yanayokuzunguka, vyote vikiwa kwenye duara, kukuzunguka wewe. Kwa lugha ya kawaida, ni tatizo la kusikia kizunguzungu. Vertigo inaweza kutokea kama mtu atachungulia chini kutoka sehemu iliyo juu sana, lakini mara nyingi tunamaanisha hali inayotokea kwa muda mfupi au kizunguzungu cha muda mrefu kutokana na dosari za sehemu ya ndani ya sikio au ubongo. Vertigo si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa. Kun