Sheria 17 za mpira wa miguu, Soka
Kila msimu mpya, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hutoa mabadiliko ya “Sheria za Mchezo” zinazoelezea kiundani taratibu za mchezo huo. Zifuatazo ni Sheria 17 za mpira wa miguu. Sheria #1: Uwanja Kuna vipimo maalumu vya viwanja wa mchezo wa soka, viwanja vidogo na vikubwa kadhalika. FIFA inasema kwamba katika mashindano ya mchezo wa soka wenye timu za wachezaji 11 kila moja, urefu wa uwanja unatakiwa uwe kati ya mita 100 na mita 130 na upana wake uwe kati ya mita 50 na 100. Kuna nafasi 11 za wachezaji kwenye uwanja wa mpira wa miguu lakini zote zinaweza kuwekwa kwenye makundi makuu manne. Kwenye michezo midogo, idadi ya wachezaji kwenye kila timu inaweza kupungua lakini nafasi hizi zinabaki kama zilivyo. Nafasi hizi kwenye mchezo wa soka ni Golikipa, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji. Sheria #2: Vipimo vya mpira Mzingo (mzunguko) wa mpira wa miguu hautakiwi kuzidi kipimo cha inchi 28 (sawa na sentimita 70) na hautakiwi kupungua inchi 27 (sawa na sentimita 68). Mpira saizi namba 5