Jinsi Ya Kupata Fedha Zaidi Kutoka Kwa Mwajiri Wako

Inabidi uwe makini kama unataka kulipwa zaidi
Ingawa kampuni nyingi zinaongezea wafanyakazi wake mishahara kila mwaka, yapo makampuni mengi ambayo hayafanyi hivyo, hivo inabidi ufanye jitihada ili kupata ongezeko la mshahara. Lakini, mazungumzo kati yako na bosi wako kuhusu kuongezewa mshahara yanaweza kuwa jambo la kuogopesha.., hii pamoja na uoga wa kukataliwa hufanya wafanyakazi wengi wasijaribu kufanya hivyo.
Lakini, kumbuka kuwa, usipojitetea utabaki na mshahara ule ule paka utakapo pandishwa cheo au kuhamia kampuni nyingine. Hivyo uwezo wa kuongea na bosi wako kwa ujasiri kuhusu ongezeko la mshahara ni maarifa muhimu ambayo yatakusaidia kwenye soko la ajira.
Je, unatakiwa ufanye nini hasa?
  1. Jua thamani yako katika soko la ajira

Ingawa unaweza kufikiri kuwa unastahili fedha nyingi zaidi ya unazopokea sasa, ongezeko la mshahara unalotaka lazima liwe na sababu. Kwa mfano kama watu wengi katika taaluma yako ambao wana uzoefu sawa wanapokea TZS 2,000,000 kwa mwezi, halafu wewe unataka TZS 4,000,000 kwa mwezi, ombi lako litaonekana halina maana ( isipokuwa pale ambapo utendaji kazi wako ni wa kipekee). Kwa ufupi, hatua ya kwanza ya kuelekea kuongezewa mshahara ni kujua thamani yako katika soko la ajira.
Kwa bahati mbaya, tunapokuja kwenye suala la mishahara, hakuna uwazi wa kutosha Tanzania, hivyo itabidi uchunguze kwa umakini. Anza kwa kuongea na watu unaojuana nao katika fani yako, wanaweza wasikwambie wao wanapokea kiasi gani, lakini watakupa kiwango cha wastani. Mtu mwingine wa kuongea nae ni Afisa Rasilimali Watu wa kampuni yako, anaweza asikwambie wafanyakazi wenzako wanapokea kiasi gani, lakini atakwambia kiwango cha wastani.
Ingawa hii ni kazi kubwa, itakusaidia kujua thamani yako ili ujue uombe kiasi gani. Unaweza kushangaa kwa kukuta kuwa unalipwa zaidi ya wenzako, au kama ilivyo kwa wengi unalipwa chini ya kiwango.
Pamoja na mshahara, unatakiwa uangalie idadi ya watu wenye ujuzi kama wako walio katika eneo lako. Ni watu wengi wenye ujuzi kama wako? Ni rahisi kupata mtu mwenye ujuzi kama wako? Au kazi yako ni ya kipekee, na ni ngumu kupata mtu mwenye ujuzi kama wako? Haya yatakujulisha kama upo kwenye nafasi nzuri ya kuomba ongezeko kubwa, au uwe mpole uombe kiasi kidogo.
  1. Ni muda sahihi?

Ingawa ni kawaida kuomba ongezeko la mshahara kila mwaka (waajiri wanalijua hili) inatakiwa pia uwe makini kwenye kupangilia ni muda gani hasa uombe ongezeko hilo.
Kitu cha kwanza unachotakiwa kuangalia ni hali ya kiuchumi ya kampuni. Kwa mfano, kama kampuni imekuwa na kipindi kigumu paka kufikia kupunguza wafanyakazi, basi huo sio muda mzuri wa kuomba kuongezewa mshahara. Lakini kama kampuni inafanya vizuri, basi ni muda unaofaa.
Zaidi, unatakiwa ujue kama ni muda mzuri wa kuongea na bosi wako. Ana shughuli nyingi anazotakiwa kumaliza haraka? Au yupo katika hali nzuri, na anaweza kuongea nawe?
Kwa ufupi, kusubiri muda mzuri ni jambo la muhimu.
  1. Onyesha maarifa yako

Hata kama wewe ni mfanyakazi kinara, bado lazima uonyeshe ni kwanini unastahili kuongezewa mshahara.  Kuonyesha hivyo, pitia kazi zote ulizofanya kwa mwaka ulioisha na angalia:
  • Kazi ulizomaliza kikamilifu na ni jinsi gani zimechangia kwenye malengo ya biashara
  • Majukumu mapya uliyonayo sasa, ambayo mwaka jana hukua nayo   
  • KPIs ulizofikia, na tathmini ulizofanyiwa
Kiujumla, unatakiwa uonyeshe umuhimu wako kwenye kampuni, uonyeshe kuwa utaendelea kufanya kazi nzuri na kuwa unastahili kuongezewa mshahara.
  1. Fanyia mazoezi ombi lako

Once you’ve got your key accomplishments written, practicing how you will present them to your boss with a friend will help build your confidence. Inform your friend of your boss’s personality ( are they friendly, serious, matter-of-fact etc.? ), so that they can imitate them to the best of their abilities.
  1. Andaa ‘Mpango B’

Mara nyingi, watu hawafikirii watafanya nini wasipopata ongezeko la mshahara. Utaacha kazi? Utaendelea kufanya kazi kwenye kampuni hiyohiyo? Unatakiwa ujue hatua yako itakayofuata. Ukiamua kuwa huwezi kundelea na kazi hiyo kwa mshahara huohuo, basi anza kutafuta kazi nyingine, kama hutopata matokeo unayotegemea.
  1. Ongea na mwajiri wako

Kama umeshafanya kazi kwenye kampuni kwa zaidi ya mwaka, basi utakuwa unajua ni njia gani nzuri zaidi ya kumufata mwajiri wako ili kupanga muda wa kuongea kuhusu ongezeko la mshahara. Waajiri wengine wanajibu barua pepe kwa haraka zaidi, wengine inabidi uongee nao uso kwa uso. Pia wengine wanapenda ujielezee kwa ufupi zaidi, wakati wengine wanapenda kusalimiana kwanza na kuongea kidogo. Funzo hapa ni kuwa, itakusaidia wewe kuongea na mwajiri yako kwa namna ambayo anapenda kuitumia.
  1. Omba maoni

Kama usipo ongezewa mshahara, muulize mwajiri wako ni nini uboreshe kwenye utendaji wako ili uweze kupata mshahara unaotaka. Hii itamuonyesha bosi wako kuwa upo tayari kufanya maboresho kwenye utendaji wako.
Lakini, kama bosi wako anashindwa kukwambia wazi nini unatakiwa uboreshe, hii ni dalili kuwa ulistahili kuongezewa mshahara lakini bosi wako sio kiongozi mzuri. Kama hii ndiyo hali halisi basi ni bora uanze kutafuta kazi nyingine.
Usijishushe thamani
Kutokana na ukosefu mkubwa wa jira, hasa kwa vijana, watu wengi wanalipwa chini ya kiwango na wanafurahi tu kuwa na kazi. Lakini, kama unafanya kazi kwa bidii, na unajua unaiongezea thamani kampuni, usiogope kuomba kuongezewa mshahara. Jiandae vizuri, kisha ongea na mwajiri wako. Kadri utakavyofanya hivi, ndio utakavyopata mshahara mkubwa katika kazi yako.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZIPATIKANAZO KWA KUTUMIA TUNGUJA PORI,NYANYA ZA MSHUMAA/CHUNGU/NGOGWE KIAFYA.

DALILI YA KUZIDI ASIDI MWILINI YOUR BODY IS ACIDIC HERE IS WHAT YOU NEED TO DO (THE REAL TRUTH BEHIND CANCER)

FAIDA YA MBOGA YA MCHICHA NI DAWA YA KUTIBU MARADHI MENGI TU UKITUMIA.